• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Wauzaji dawa duni za mifugo waonywa Tanzania

    (GMT+08:00) 2018-12-03 20:12:40

    Naibu waziri wa afya nchini Tanzania Dk Faustine Ndugulile amewaonya wafanyabiashara walaghai dhidi ya kuuza dawa za mifugo za ubora wa chini.

    Amesema tatizo la masalia ya dawa kwenye nyama, maziwa na mayai yanatokana na wafugaji kutozingatia matumizi ya kutoa dawa kwa mifugo yao au kutoa dawa duni.

    Dk Ndugulile amesema jitihada zinahitajika kutokomeza tatizo hilo kabla halijaleta athari kubwa zaidi.

    Ameitaka pia Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kuongeza uwezo wa kimaabara katika kuchunguza bidhaa zote zinazoingizwa sokoni pamoja na zile zinazoingizwa toka nje ya nchi ili ziwe na viwango stahiki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako