• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Shenzhen Half Marathon: Mamia watumia njia ya mkato katika mbio za riadha, China

  (GMT+08:00) 2018-12-04 08:44:34
  Wanariadha takribani 250 waliokuwa wanashiriki mbio fupi za riadha (half marathon) nchini China walinaswa na kamera za siri wakitumia njia ya mkato kumaliza mbio hizo.

  Wengi walipitia vichakani na wengine kwenye vichochoro. Waandalizi wa mbio hizo zilizofanyika mjini Shenzhen, wamesema waligundua pia wakimbiaji 18 waliokuwa wamevalia vibango vya nambari za kuwatambua wanariadha vilivyokuwa bandia.

  Kulikuwa pia na wanariadha watatu ambao wameelezwa kuwa wanariadha feki waliokuwa wanajifanya kuwa watu tofauti.

  Waandalizi wa mashindano hayo wamesema, wanariadha wote waliopatikana wamefanya udanganyifu huo sasa wanakabiliwa na uwezekano wa kupigwa marufuku.

  China imeandaa mashindano 1,072 ya marathon na mbio nyingine za nyika mwaka huu, idadi hii ikiwa imeongezeka kutoka 22 mwaka 22, kwa mujibu wa Chama cha Riadha cha China.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako