• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bibi Peng Liyuan akutana na mke wa rais wa Panama

    (GMT+08:00) 2018-12-04 08:53:39

    Mke wa rais wa China Bibi Peng Liyuan na mwenzake wa Panama Bibi Lorena Castillo Garcia de Varela wamekutana na kuhudhuria shughuli za matangazo ya umma kuhusu kinga na tiba ya ugonjwa wa UKIMWI katika ikulu ya Panama.

    Bibi Peng ambaye ni balozi wa heshima wa Shirika la Afya Duniani WHO kuhusu maradhi ya kifua kikuu na UKIMWI na balozi wa Shirika la Elimu, Sayansi, Elimu na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO kuhusu kuhimiza elimu ya wasichana na wanawake, amesema serikali ya China inatilia maanani na kufanya juhudi kubwa katika kazi za kinga na tiba ya ugonjwa wa UKIMWI, na kuinua kiwango cha elimu kwa wanawake na watoto. Ameeleza matumaini yake kuwa nchi hizo mbili zitashirikiana kutoa mchango mkubwa zaidi katika kuhimiza shughuli zinazohusu wanawake na wasichana wa nchi hizo mbili na wa dunia nzima.

    Bibi Castillo amesema Panama inapenda kushirikiana na China ili ushirikiano kati ya nchi hizi mbili katika shughuli hizo upate maendeleo zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako