• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia yazindua kampeni ya taifa ya kutoa chanjo ya HPV kwa wasichana

    (GMT+08:00) 2018-12-04 09:01:50

    Wizara ya afya ya Ethiopia imezindua kampeni ya taifa ya kutoa chanjo dhidi ya virusi vya HPV kwa wasichana milioni 1.1 nchini humo katika mwaka huu wa fedha, ili kuwakinga dhidi ya saratani ya shingo ya uzazi.

    Akiongea kwenye uzinduzi wa programu hiyo, waziri wa afya wa Ethiopia Bw. Amir Aman amesisitiza kuwa saratani ya shingo ya uzazi ni ugonjwa unaozuilika, endapo wasichana watapewa chanjo ipasavyo.

    Shirika la afya duniani WHO limeyatambua maambukizi ya virusi vya HPV kuwa ni chanzo kikuu cha matukio 68,000 ya saratani ya shingo ya uzazi yanayotokea kila mwaka barani Afrika, na wanawake 23 kati ya kila wanawake laki moja, wanafariki kutokana na saratani hiyo kila mwaka barani humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako