• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ujenzi wa barabara kuu kati ya Kenya na Tanzania kuanza mapema mwaka 2019

    (GMT+08:00) 2018-12-04 09:12:04

    Benki ya maendeleo ya Afrika (AfDB) imesema ujenzi wa barabara kuu ya eneo la pwani itakayounganisha mji wa pwani wa Kenya wa Malindi na mji wa pwani wa Tanzania, Bagamoyo, unatarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwaka 2019.

    Mkurugenzi wa ofisi ya maendeleo na biashara ya benki hiyo katika eneo la Afrika Mashariki Bw. Gabriel Negatu, amesema benki hiyo itatoa asilimia 70 ya gharama za ujenzi wa barabara hiyo, huku Kenya na Tanzania zikitoa asilimia 30 kwa mujibu wa maeneo ya nchi zao.

    Bw. Negatu amesema wanatoa kipaumbele kwa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 460, kati ya hizo 250 zikiwa upande wa Tanzania, ambayo itahimiza biashara ya kikanda. Ujenzi wa barabara hiyo inayotarajiwa kurahisisha usafirishaji wa bidhaa kutoka bandari za Mombasa na Bagamoyo, unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 36.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako