• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda imesimamisha makampuni 197 kufanya biashara na serikali kutokana na kukiuka mikataba na udanganyifu

    (GMT+08:00) 2018-12-04 09:12:24

    Rwanda imesimamisha kufanya biashara na makampuni 197 kutokana na kukiuka mikataba na kufanya udanganyifu wakati wa kuomba zabuni. Mamlaka ya manunuzi ya umma ya Rwanda imesema makampuni hayo hayana sifa tena ya kufanya biashara na serikali.

    Mkurugenzi wa mamlaka hiyo Bw. Augustus Seminga, amesema idara zote za manunuzi ya umma haziruhusiwi kutoa kandarasi, zabuni au kufanya biashara na makampuni hayo, katika kipindi chote cha kusimamishwa. Hata hivyo amesema uamuzi huo unaweza kupingwa mahakamani.

    Ripoti ya mkaguzi wa mahesabu ya serikali ya mwaka wa fedha uliopita, inasema wakandarasi walichelewesha au kutelekeza miradi 109 yenye thamani ya dola 235 za kimarekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako