• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika kuwa juu kwenye ajenda ya Baraza la Usalama baada ya Cote d'Ivoire kushika uenyekiti Disemba

    (GMT+08:00) 2018-12-04 09:45:36

    Afrika itakuwa juu kwenye ajenda ya mpango wa kazi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwezi Disemba baada ya Cote d'Ivoire kushika uenyekiti wa zamu wa mwezi huu wa Baraza hilo. Balozi wa Cote d'Ivoire kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Leon Adom amesema kutakuwa na mdahalo miongoni mwa wajumbe wa Baraza la Usalama kesho kuhusu ujenzi mpya baada ya mgogoro, utakaohudhuriwa na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guteterres na mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako