• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bei za mafuta zaimarika baada ya Marekani na China kukubaliana kuacha kuongeza ushuru na Qatar kujitoa OPEC

    (GMT+08:00) 2018-12-04 09:46:25

    Bei za mafuta zimeongezeka baada ya China na Marekani kukubaliana kutoongezeana ushuru mpya kwa bidhaa za upande mwingine, na Qatar kuamua kujitoa kwenye Shirika la Nchi Zinazouza Mafuta kwa Wingi OPEC. Wachambuzi wanasema masoko ya mafuta yamehamasishwa na kuongezeka kwa imani za wawekezaji kufuatia mazungumzo mazuri kati ya marais wa China na Marekani ambayo yamezidi matarajio. Wakati huohuo, waziri wa nishati wa Qatar Bw. Saad al-Kaabi amesema nchi hiyo haitajitoa kwenye sekta ya mafuta, ila sekta hiyo inaongozwa na Shirika moja linalodhibitiwa na nchi moja, yaani Saudi Arabia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako