• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kongamano la kwanza la biashara kati ya China na Afrika lafanyika Addis Ababa

    (GMT+08:00) 2018-12-04 09:55:27

    Kongamano la kwanza la biashara kati ya China na Afrika lilifanyika jana mjini Addis Ababa, Ethiopia.

    Kongamano hilo la siku tatu lenye lengo la maonesho ya ushirikiano wa viwanda wa China na Ethiopia, lina shughuli nyingi zikiwemo, maonyesho ya ngazi ya juu ya biashara, kongamano la ushirikiano wa viwanda, mkutano wa kuhimiza uwekezaji na matembezi katika bustani za kiviwanda za Ethiopia.

    Mwenyekiti wa Shirika la biashara la Ethiopia ECCSA Bw. Melaku Ezezew amesisitiza uhusiano mzuri wa kibiashara na kiserikali kati ya China na Ethiopia, na kusema kongamano hilo litatoa fursa kwa makampuni kuanzisha wenzi wa ushirikiano kati yao. Makampuni 46 ya China yameshiriki na kuonesha bidhaa na huduma zao katika kongamano hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako