• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa uchumi wa Afrika kufuatilia vizuizi vya mafungamano Afrika

    (GMT+08:00) 2018-12-04 09:56:33

    Maofisa wanaohudhuria mkutano wa uchumi wa Afrika unaofanyika mjini Kigali, wenye lengo la kutafuta njia ya kuondoa vizuizi kwenye mafungamano ya Afrika wamesisitiza umuhimu wa ushirikiano katika maendeleo ya Afrika .

    Mkutano wa 13 wa mwaka utakaofunguliwa Jumatano utafuatilia hatua za kuharakisha maendeleo ya kasi katika ushirikiano wa miundo mbinu, pamoja na kuondolewa kwa vizuizi kwa watu, bidhaa na huduma kwenye mipaka ya nchi.

    Habari pia zinasema mkurugenzi mkuu wa ofisi ya biashara na maendeleo ya eneo la Afrika Mashariki ya benki ya maendeleo ya Afrika Bw. Gabriel Negatu alipohojiwa kwenye mkutano huo amesema Afrika inakaribisha uwekezaji binafsi kutoka China hasa katika sekta za uchukuzi, nishati na maendeleo ya viwanda, ambao utaisaidia Afrika kuhimiza utekelezaji wa biashara huria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako