• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pakistan yapenda kusaidia kuratibu kundi la Taliban kujiunga na mazungumzo ya amani ya Afghanistan

    (GMT+08:00) 2018-12-04 17:02:16

    Waziri mkuu wa Pakistan Bw. Imran Khan amesema, nchi hiyo inapenda kusaidia kuratibu kundi la Taliban kujiunga na mazungumzo ya amani na Afghanistan.

    Bw. Khan amesema hayo wakati mjumbe maalum wa Marekani anayeshughulikia na suala la Afghanistan Bw. Zalmay Khalilzad akiwasili nchini humo kwa mazungumzo ya kutafuta suluhisho la kisiasa kwa migogoro ya Afghanistan.

    Vyombo vya habari vimemnukuu Bw. Imran Khan akisema, rais wa Marekani Donald Trump amemwandikia barua akieleza matarajio yake kuwa Pakistan itaonesha ushawishi wake katika kulirejesha kundi la Taliban la Afghanistan kwenye meza ya mazungumzo ya mchakato wa amani.

    Wizara ya mambo ya nje ya Paskistan imesema, mambo muhimu yaliyozingatiwa na Marekani kwenye barua hiyo ni kumaliza vita nchini Afghanistan na kufikia makubaliano kwa njia ya mazungumzo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako