• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uhusiano kati ya China na Ureno wafungua ukurasa mpya

  (GMT+08:00) 2018-12-04 17:10:20

  Kutokana na mwaliko wa rais Marcelo Rebelo de Sousa wa Ureno, rais Xi Jinping wa China leo ameanza ziara rasmi nchini Ureno. Hii ni mara ya kwanza kwa rais wa China kufanya ziara chini humo katika miaka minane iliyopita. Wakati China na Ureno zinapokaribisha maadhimisho ya miaka 40 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya pande hizo mbili, ziara hiyo ya rais Xi itafungua ukurasa mpya wa maendeleo ya uhusiano kati ya pande hizo mbili.

  Ingawa China na Ureno zinatofautishwa kwa umbali mkubwa kati yao, uhusiano wa kisiasa, ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara na mawasiliano ya utamaduni kati ya pande hizo mbili umekuwa ukiendelea vizuri. Hivi sasa uwekezaji wa China nchini Ureno umezidi EURO bilioni 9 ambao unahusisha nyanja za nishati, fedha, bima, TEHAMA, usafiri wa ndege za abiria, usimamizi wa mambo ya maji, usanifu na vifaa vya ujenzi, afya, na matibabu, na kutoa nafasi zaidi ya elfu 36 za ajira kwa wakazi wa huko.

  Kutokana na habari zilizotolewa na serikali ya Ureno, wakati wa ziara ya kwanza ya rais Xi Jinping nchini Ureno, pande hizo mbili zitatoa taarifa ya pamoja kuhusu uhusiano kati ya pande hizo mbili, na kusaini makubaliano ya awali kuhusu ushirikiano wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" pamoja na makubaliano mbalimbali ya ushirikiano, ambayo yataonesha umuhimu mkubwa katika kuimarisha maendeleo ya uhusiano wa kiwenzi na kimkakati wa pande zote kati ya pande hizo mbili, na kuzidi kukuza uhusiano wa ushirikiano kati ya China na Umoja wa Ulaya.

  Mbali na hayo, China na Ureno vilevile zinaimarisha ushirikiano na nchi nyingine zinazozungumza lugha za kireno. Kutokana na sababu za kihistoria, hivi sasa kuna nchi 9 zenye idadi ya watu milioni 250 wanaozungumza kireno duniani zikiwa ni pamoja na Ureno, Brazil na Angola, na zimeanzisha Jumuiya ya nchi za kireno na kufanya ushirikiano wa kisiasa na kiuchumi pamoja na mawasiliano ya kijamii. Ushirikiano kati ya China na Ureno umepanuka hadi katika nchi nyingine zinazozungumza kireno.

  Hivi sasa muundo wa dunia unakabiliwa na changamoto kubwa, na uhusiano kati ya China na Ulaya unahitaji msukumo mpya. Wakati utekelezaji wa pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" bado haujakamilika, ziara hiyo ya rais Xi Jinping si kama tu itafungua ukurasa mpya kwa maendeleo ya uhusiano kati ya pande hizo mbili, bali pia italeta msukumo mpya kwa uhusiano kati ya pande hizo mbili, ili kuchangia kufufuka kwa uchumi wa dunia na utulivu wa hali ya kimataifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako