• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa China awasili Ureno kwa ziara ya kiserikali

  (GMT+08:00) 2018-12-04 18:22:02

  Rais Xi Jinping wa China amewasili nchini Ureno kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili inayolenga kuendeleza urafiki na kupanua ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

  Hii ni ziara ya kwanza kufanywa na mkuu wa nchi ya China nchini Ureno katika miaka minane iliyopita.

  Rais Xi amesisitiza kuwa, mwaka kesho utakuwa mwaka wa 40 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya China na Ureno, ambao ni mwanzo mpya wa kihistoria wa maendeleo ya uhusiano wa pande hizo mbili. Katika ziara hiyo, rais Xi anatarajia kukutana na viongozi wa Ureno na kuweka mipango kuhusu mustakabali wa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili. Pia anaamini kuwa kutokana na juhudi za pamoja za pande hizo mbili, uhusiano wa kiwenzi na kimkakati wa pande zote utapata maendeleo mapya katika siku za baadaye.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako