• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Hafla ya uzinduzi wa sanamu ya Mandela yafanyika Beijing

  (GMT+08:00) 2018-12-04 18:35:53

  Hafla ya uzinduzi wa sanamu ya aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Nelson Mandela imefanyika mjini Beijing, China.

  Huu ni mwaka wa 20 tangu China na Afrika Kusini zianzishe uhusiano wa kibalozi, na pia ni mwaka wa 100 tangu Mandela azaliwe. Waziri wa sanaa na utamaduni wa Afrika Kusini Bw. Nkosinathi Emmanuel Mthethwa alipohutubia hafla hiyo amesema, sanamu hiyo ni kwa ajili ya kukumbusha moyo wa Mandela wa kulinda heshima ya binadamu na kujenga utaratibu wa kimataifa wenye usawa na haki. Amesema, Mwaka 1964, wakati Mandela na wenzake walipohukumiwa kifungo cha maisha, China ilikuwa moja kati ya nchi zilizoulaumu utawala wa Afrika Kusini. Baada ya Mandela kuachiwa huru, China pia ilikuwa moja ya nchi ambazo Mandela alifanya ziara mapema zaidi. Kutokana na uhusiano wa kihistoria kati ya Afrika Kusini na China, Mandela alitangaza kufuata sera ya kuwepo kwa China moja duniani, na kuanzisha uhusiano wa kibalozi kati ya nchi hizo mbili tarehe mosi, Januari mwaka 1998. Ameongeza kuwa Afrika kusini inashukuru China na wananchi wake kwa kutoa uungaji mkono kwa ajili ya juhudi za Afrika Kusini kujipatia ukombozi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako