• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Watumiaji wa Mpesa kutuma pesa moja kwa moja hadi China

  (GMT+08:00) 2018-12-04 20:48:03
  Watumizi wa M-Pesa sasa wanaweza kutuma pesa moja kwa moja hadi Uchina kwa kutumia mtandao mkubwa zaidi nchnii humo, WeChat. Biashara hiyo imewezeshwa na Family Bank ikishirikiana na SimbaPay, ambayo ina makao yake jijini London.

  Ili kutuma pesa, Wakenya watatumia nambari ya kutuma inayomilikiwa na Family Bank ambapo namba ya simu ya wanaotaka kutumia ndio nambari ya akaunti.

  Mpokeaji atapata pesa hizo katika mfuko wa simu yao. Gharama kutuma itakuwa tofauti kuambatana na kiwango cha pesa ulichotuma. Kwa mfano, kutuma Sh8,198 itagharimu Sh350.

  Pia, wateja wanaweza kutumia PesaPap au huduma ya ujumbe kwa nambari iliyotambulishwa na benki hiyo kutuma pesa kwa WeChat.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako