• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bunge la Afrika Kusini lapitisha mchakato wa kufanya marekebisho ya katiba kwa ajili ya mageuzi ya ardhi

    (GMT+08:00) 2018-12-05 09:04:27

    Baraza la chini la bunge la Afrika Kusini limepitisha uamuzi wa kukifanyia marekebisho kifungu cha 25 cha katiba, ili kufanya utwaaji wa ardhi bila fidia kuwa wazi zaidi.

    Bunge hilo limepitisha ripoti iliyowasilishwa na kamati ya mapitio ya katiba, inayotaka kuwekwa wazi utwaaji wa ardhi bila fidia kwa manufaa ya umma, kama njia moja ya kurekebisha dhuluma zilizotokea huko nyuma kwa waafrika kusini walio wengi.

    Ripoti hiyo imeidhinishwa na wabunge 209 na kupingwa na watu 91. Hata hivyo wabunge wametoa angalizo kuwa utwaaji ardhi huo, unatakiwa kufanywa kwa njia ya kushughulikia dhuluma za zilizofanywa zamani.

    Ripoti hiyo sasa inapelekwa kwenye baraza la juu ili kupitiwa, na kama ikipitishwa, kutwaa ardhi bila fidia kutakuwa sheria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako