• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri Mkuu wa Uingereza afanya juhudi za mwisho kulishawishi bunge kukubali mpango wake wa Brexit

  (GMT+08:00) 2018-12-05 09:04:50

  Waziri Mkuu wa Uingereza Bibi Theresa May jana alifanya juhudi za mwisho kuwashawishi wabunge wa Uingereza kuunga mkono mpango wake wa Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya yaani Brexit, siku chache kabla ya upigaji kura kufanyika tarehe 11 Desemba.

  Bibi May amesisitiza kuwa mpango wake wa Brexit uliofikiwa kati ya serikali yake na Umoja wa Ulaya, ni chaguo pekee lililo mbele ya bunge, na kusema chaguo kwa wabunge ni makubaliano haya, au kutokuwa na makubaliano au kutojitoa Umoja wa Ulaya.

  Bibi May amesema mgawanyo kutokana na Brexit umekuwa mbaya kwa siasa za Uingereza, na Umma unaona kuwa siasa zake zimechukua muda mrefu sana. Amesema upigaji kura za maoni wa pili utaleta mgawanyo zaidi, kwa nchi ambayo imegawanyika tangu upigaji kura wa kwanza uliofanyika mwaka 2016.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako