• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Afrika iko nyuma katika kutuma raslimali zake kwa maendeleo

  (GMT+08:00) 2018-12-05 09:06:34

  Ripoti kuhusu Maendeleo Endelevu ya Afrika kwa mwaka 2018 iliyotolewa jana mjini Kigali nchini Rwanda imesema Afrika iko nyuma katika kugeuza maliasili yake kuwa matokeo halisi ya maendeleo.

  Ripoti hiyo iliyoandaliwa kwa pamoja na Umoja wa Afrika, Kamisheni ya uchumi wa Afrika ya Umoja wa mataifa na Shirika la maendeleo la Umoja wa mataifa UNDP, ilipitia juhudi za kuboresha usimamizi wa maliasili za Afrika, haswa hitaji la kuimarisha taasisi za usimamizi wa maliasili na taratibu za kuboresha ukusanyaji wa mapato ya ndani.

  Ripoti inasema sekta ya maliasili inaipatia Afrika uwezo wa kuchochea maendeleo na kutoa msingi wa kiraslimali kwa ajili ya maendeleo ya kifedha, lakini inakabiliwa na changamoto nyingi, hali inayowahitaji wadau wote wakiwemo serikali, sekta binafsi na jumuiya za kiraia, kujihusisha kwenye mageuzi ya usimamizi wa maliasili.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako