• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Afrika yahitaji sera bora ya viwanda ili kuhimiza uuzaji nje wa bidhaa za viwandani

  (GMT+08:00) 2018-12-05 09:06:54

  Wachumi wamezihimiza nchi za Afrika kuongeza ufanisi wa sera zao za viwanda ili kuhimiza uuzaji nje wa bidhaa za viwandani, wakati bara hilo linasukuma mbele mafungamano ya kikanda kwa ajili ya kuhimiza biashara.

  Akiongea kwenye kikao kimoja kwenye Mkutano wa uchumi wa Afrika uliofanyika mjini Kigali, Rwanda, mchumi wa Kamisheni ya uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa Bw. Rodgers Mukwaya, amesema nchi za Afrika zinahitaji kuzifanya sera zao za viwanda ziwe na ufanisi zaidi kutokana na umaalumu wa kiuchumi na fursa za kuhimiza uuzaji nje wa bidhaa za viwandani.

  Mchumi wa Shirika la maendeleo la Umoja wa mataifa UNDP Bibi Janvier Alofa, amesema ukosefu wa sera za viwanda zenye ufanisi barani Afrika umezuia ukuaji wa uuzaji nje wa bidhaa za viwandani, na kuzifanya nchi nyingi za Afrika zitegemee uagizaji bidhaa kutoka nje.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako