• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Klabu bingwa Afrika: Simba SC yaifumua Mbabane Swallows 8-1

  (GMT+08:00) 2018-12-05 09:12:41
  Simba Sports Club ya Tanzania imeingia hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania kushiriki hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya wenyeji, Mbabane Swallows jioni ya jana uwanja wa Mavuso mjini Manzini, Eswatini, zamani Swaziland.

  Simba inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 8-1, baada ya kushinda 4-1 kwenye mchezo wa kwanza wa raundi ya awali ya mchujo Jumatano ya wiki iliyopita uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

  Simba SC sasa itakutana na mshindi wa jumla wa mchezo kati ya UD Songo ya Msumbiji au Nkana FC ya Zambia zinazorudiana leo uwanja wa Nkana mjini Kitwe Zambia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako