• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Kombe la Shirikisho barani Afrika: Wakatamiwa wa Turiani waifungashia virago Northern Dynamos

  (GMT+08:00) 2018-12-05 09:13:05
  Timu ya Mtibwa Sugar aka wakatamiwa wa Turiani ya Tanzania imefanikiwa kwenda raundi ya pili ya mchujo wa kuwania kucheza hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Northen Dynamo mchezo uliochezwa jana jioni uwanja wa Linite, Glacis kisiwa cha Mahe nchini Shelisheli.

  Kwa ushindi huo uliotokana na bao pekee la kiungo Haroun Chanongo, Mtibwa Sugar inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 5-0, baada ya kushinda 4-0 kwenye mchezo wa kwanza uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam.

  Sasa Mtibwa Sugar itamenyana na KCCA ya Uganda inayoanzia raundi ya kwanza na mechi ya kwanza itafanyika Desemba 14 mjini Kampala kabla ya timu hizo kurudiana wiki moja baadaye Dar es Salaam.

  Kwa upande wa wawakilishi wa Zanzibar kwenye kombe la shirikisho, Zimamoto wametupwa nje licha ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kaizer Chiefs mchezo uliopigwa jana uwanja wa Amani, kisiwa cha Unguja.

  Zimamoto inatupwa nje kwa jumla ya mabao 5-2 baada ya kufungwa 4-0 kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita Port Elizabeth Afrika Kusini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako