• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudani Kusini kushiriki mashindano ya Olimpiki maalum ya wenye ulemavu mwaka 2019

    (GMT+08:00) 2018-12-05 09:13:25
    Sudan Kusini inatarajiwa kushiriki michuano maalum ya watu wenye ulemavu ya Olimpiki msimu wa joto mwezi Machi mwakani yatakayofanyika Abu Dhabi ikiwa ni njia ya kuhamasisha haki za watu wenye ulemavu.

    Rais wa kamati ya Olimpiki nchini humo bwana Juma Stephen Lugga ameeleza kuwa wanamichezo wengi wenye ulemavu katika nchi za Afrika mashariki hawapewi sapoti ya kutosha na kuachwa nyuma katika masuala ya michezo kutokana na ulemavu walionao.

    Amesema kamati ya olimpiki ya Sudan Kusini imeanza kuchagua wanariadha watakaowakilisha nchi hiyo kwenye michuano hiyo mwakani.

    Sudan kusini ilipata uanachama wa kamati ya olimpiki ya kimataifa (IOC) mwezi Agosti mwaka 2015.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako