• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makampuni ya China yaongeza ajira kwa wazawa Kenya

    (GMT+08:00) 2018-12-05 14:01:29

    Makampuni ya China nchini Kenya yanaendelea na mpango wake wa kuhakikisha yanatoa ajira zaidi kwa wazawa wa Kenya.

    Ofisa wa ubalozi wa China nchini Kenya Bw. Li Xuang amesema makampuni ya China yameamua kushirikiana zaidi na wenyeji, kwa kuwa yanatambua kuwa waajiriwa wakenya ni wachapakazi, wenye dhamira na wanaoona mbali, na wanaweza kujitahidi kukabiliana na tofauti za kitamaduni na lugha ili kuwa na mafanikio.

    Bw. Li Xuhang amesema hayo katika sherehe ya kutoa tuzo ya wafanyakazi bora ya Shirika la uchumi na biashara kati ya China na Kenya (KCETA), ambapo wafanyakazi 55 wanaofanya kazi katika makampuni ya China walitunukiwa tuzo hiyo kutokana na jitihada zao za muda mrefu. Bw. Li pia amesema, kuanzia mwaka 2016 hadi mwaka huu shirika hilo limeongeza idadi ya ajira kwa wazawa wa Kenya kutoka elfu 42 hadi elfu 50.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako