• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Emir wa Qatar apokea mwaliko kutoka mfalme wa Saudi Arabia kushiriki kwenye mkutano wa kilele wa GCC

  (GMT+08:00) 2018-12-05 10:01:07

  Shirika la habari la Qatar limesema Emir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al-Thani amepokea mwaliko kutoka kwa mfalme Salman wa Saudi Arabia kushiriki kwenye mkutano wa 39 wa kilele wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba unaotarajiwa kufanyika tarehe 9, Disemba mjini Riyadh. Shirika hilo halikusema kama Emir atakubali mwaliko au la. Mwaliko huo umekuja wakati tofauti kati ya Qatar na nchi jirani zake zinaongezeka tangu Juni, mwaka 2017 ambapo Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain na Misri zilisimamisha uhusiano wa kibalozi na Qatar.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako