• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda yahimizwa kushawishi Umoja wa Afrika kuwaangamiza waasi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

    (GMT+08:00) 2018-12-05 10:05:36

    Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa Kanda ya Maziwa Makuu Bw. Said Djinnit ameihimiza Uganda kuushawishi Umoja wa Afrika na mashirika mengine ya kikanda kuwaondoa waasi walioko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC.

    Bw. Djinnit aliyasema hayo jana alipokutana na waziri wa mambo ya nje wa Uganda Bw. Sam Kutesa. Amesema Umoja wa Afrika na mashirika mengine ya kikanda yakiwemo Mkutano wa Kimataifa kuhusu mambo ya Kanda ya Maziwa Makuu na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC, zinapaswa kushirikiana vizuri ili kuwaangamiza waasi wa kundi la Allied Democratic Force ADF na kuwarudisha wapiganaji wa M23.

    Bw. Kutesa amesema Uganda itafanya ushirikiano kuhusu mchakato huu, na pia inataka Umoja wa Mataifa kuzihamasisha nchi nyingine kujiunga na mchakato huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako