• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa Afrika Kusini ataka nchi za BRICS kufanya juhudi kukuza uchumi

  (GMT+08:00) 2018-12-05 10:05:58

  Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amezitaka nchi za BRICS kufanya juhudi kuhimiza ongezeko la uchumi na kuboresha maisha ya watu.

  Rais Ramaphosa aliyasema hayo kwenye mkutano wa vyama vya kisiasa vya nchi za BRICS uliofanyika jana mjini Pretoria. Alihamasisha viongozi wa nchi za BRICS kujitahidi kuwa na mtazamo wa kusonga mbele ili kukabiliana na changamoto za kimataifa. Pia alisisitiza nchi za BRICS kujishughulisha kulinda utaratibu wa biashara ya pande nyingi, wenye haki na uwazi. Alisema nchi hizo zinapaswa kuhimiza maendeleo shirikishi kwa kutumia mbinu za sera, na kuongeza mazungumzo ya lazima ili kuimarisha imani ya dunia kuhusu ongezeko la uchumi.

  Rais Ramaphosa pia amezitaka nchi za BRICS ziendeleze uchumi na kuboresha maisha ya watu kutokana na maendeleo ya teknolojia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako