• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China kuongeza nguvu katika kuvisaidia viwanda vidogo na vya watu binafsi

  (GMT+08:00) 2018-12-05 16:45:29

  Naibu waziri wa raslimali watu na utoaji wa huduma za jamii Bibi Zhang Yizhen amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari kuwa kwenye Ofisi ya habari ya Baraza la serikali la China, kuwa mwaka huu hali ya jumla ya utoaji wa nafasi za ajira imeonesha hali ya utulivu, na China itaongeza nguvu katika kuvisaidia viwanda vidogo na vyenye ukubwa wa kati, pamoja na viwanda vya watu binafsi.

  Bibi Zhang Yizhen amesema, mwaka huu 2018 hali ya jumla ya utoaji wa nafasi za ajira inaendelea kwa utulivu, huku utoaji wa nafasi hizo ukiongezeka kwa hatua madhubuti.

  "Mwaka huu kati ya mwezi Januari na Oktoba utoaji wa nafasi za ajira umeongezeka na kufikia milioni 12, kiasi ambacho kimeongezeka kwa watu elfu 90 kuliko mwaka jana wakati kama huu; mwezi Oktoba kiwango cha watu wasio na ajira kote nchini kilikuwa asilimia 4.9 ambacho kinalingana na mwaka jana wakati kama huu; katika robo ya tatu kwa mwaka huu, kiwango cha watu wasio na ajira kote nchini kilipungua hadi kufikia asilimia 3.82 ambacho ni kiwango cha chini zaidi katika miaka ya hivi karibuni. Pili, kiwango cha upatikanaji wa ajira cha wanafunzi waliohitimu vyuo vikuu kiko kwenye hali yenye utulivu, kiwango hicho cha nguvu kazi ya watu wanaohamia mijini kutoka vijijini kinapata maendeleo kwa hatua madhubuti, na utoaji wa misaada kwa watu wenye matatizo kiuchumi unaongezeka. Tatu, kiwango cha utoaji kinazidi mahitaji ya ajira katika soko la nguvu kazi."

  Bibi Zhang Yizhen pia asisitiza kuwa, inapaswa kuzingatia athari mbaya zinazoletwa na kuzorota kwa uchumi na mgogoro wa biashara. Ili kuzidi kuhimiza utoaji wa nafasi za ajira, baraza la serikali la China limetangaza sera inayohusika ya kuunga mkono maendeleo ya viwanda, kuhimiza utoaji wa nafasi za ajira na kuanzisha biashara, na kuwasaidia wafanyakazi waliopunguzwa kazini. Waraka huo pia unatarajiwa kuongeza nguvu katika kuviunga mkono viwanda vya watu binafsi na viwanda vidogo. Bibi Zhang Yizhen anasema:

  "China imeongeza nguvu katika kuchangisha fedha na kutoa bima kwa viwanda vidogo, kuhamasisha sehemu mbalimbali kutoa msaada kwa viwanda vidogo na vya watu binafsi, na pia kuongeza nguvu katika kutoa mikopo kwa watu wanaoanzisha biashara."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako