• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Timu ya majadiliano ya serikali ya Yemen yaelekea nchini Sweden kushiriki kwenye mazungumzo ya amani

  (GMT+08:00) 2018-12-05 18:48:08

  Timu ya majadiliano inayowakilisha serikali ya Yemen inayoungwa mkono na Saudi Arabia imeondoka nchini humo kuelekea Sweden kushiriki kwenye mazungumzo ya amani yanayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa.

  Timu hiyo ya watu 13 inayoongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Yemen Bw. Khaled Yamani, inakwenda nchini Sweden kufanya majadiliano ya moja kwa moja na ujumbe wa waasi wa Houthi.

  Majadiliano kati ya pande hizo mbili nchini Sweden yanatarajiwa kufuatilia zaidi kuruhusu watu wa Yemen kupata misaada ya kibinadamu, kutokana na tishio kubwa la njaa na vita inayoendelea.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako