• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkuu wa IMF atoa wito wa kujenga upya biashara ya pande nyingi

    (GMT+08:00) 2018-12-05 19:05:04

    Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Bi. Christine Lagarde amezitaka nchi mbalimbali kufikiria upya ushirikiano wa kimataifa na kwa pamoja kujenga upya mfumo wa biashara ya pande nyingi.

    Akizungumza katika ukumbi wa Maktaba wa bunge la Marekani mjini Washington, Bi. Lagarde amesema ushirikiano wa kimataifa ni muhimu, na sio jambo la kufanya uamuzi. Akirejea historia ya taasisi za Bretton Woods zilizoanzishwa baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia, ambazo zinajumuisha Benki ya Dunia na IMF, Bi Lagarde amesema mfumo huo wa uratibu ulikuwa wa kimapinduzi na uliona mbali. Lakini amesema katika zama hizi hali imebadilika kutokana na sababu kadhaa ikiwemo siasa za kijiografia na kuhama kwa nguvu za kiuchumi, pia uvumbuzi wa kiteknolojia, na mabadiliko hayo yanaweza kuleta fursa kubwa lakini pia hatari zisizotarajiwa.

    Bi. Lagarde amependekeza nchi mbalimbali kuboresha ushirikiano wa kiuchumi katika maeneo manne makubwa, ambayo ni biashara, ushuru wa kimataifa, mabadiliko ya hali ya hewa, na ufisadi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako