• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Lebanon ataka jeshi la nchi hiyo kufuatilia hali ya mpaka kati yake na Israel

    (GMT+08:00) 2018-12-05 19:15:46

    Rais Michel Aoun wa Lebanon ameamuru jeshi la nchi hiyo na idara za usalama kufuatilia hali ya eneo la mpaka kati yake na Israel kusini mwa nchi hiyo.

    Taarifa ilioyotolewa na Ikulu ya Lebanon imesema, baada ya Israel kutangaza kufanya operesheni ya ngao ya kaskazini kuharibu mahandaki ya kuvuka mpaka yaliyojengwa na kundi la Hezbollah la Lebanon, rais Aoun amefuatilia maendeleo ya hali ya mpaka huku akifanya maongezi ya simu na spika wa bunge, waziri mkuu na mkuu wa jeshi wa nchi hiyo ili kutathmini hali kutokana na habari kuhusu ukubwa wa operesheni ya Israel.

    Jeshi la Lebanon pia limetoa taarifa ikisema, hali ya upande wa nchi hiyo bado ni tulivu. Chini ya ushirikiano na uratibu wa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini humo, jeshi hilo litafanya operesheni mpakani kama kawaida, na kwamba limejitayarisha kukabiliana na mgogoro wowote utakaoweza kutokea katika eneo hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako