• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yataka kuhimiza maendeleo ya uhusiano kati yake na Marekani kwa kufuata makubaliano ya marais wa nchi hizo mbili

    (GMT+08:00) 2018-12-05 19:16:24

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, China inaitaka Marekani kuelekea upande mmoja na China, ili kuhimiza maendeleo ya uhusiano kati ya pande hizo mbili kwa kufuata makubaliano ya marais wa nchi hizo na kuleta manufaa halisi kwa watu wa nchi hizo mbili na dunia kwa ujumla.

    Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Mike Pompeo huko Brussels amesema, Marekani haitaki kukubali kitendo cha China, Iran na Russia kukiuka makubaliano na mikataba ya pande nyingi. Ameongeza kuwa Marekani itachukua hatua kufanya mageuzI kwa mashirika ya kimataifa ikiwemo Umoja wa Mataifa, IMF na Benki ya Dunia.

    Bw. Geng amesema, hoja mpya ya Marekani haiendani na nia ya mkutano wa marais wa China na Marekani, ambao siku kadhaa zilizopita, walifikia makubaliano muhimu katika mkutano wa kilele wa G20. Mbali na suala la uchumi na biashara linalofuatiliwa na pande nyingi, pande hizo mbili zimekubaliana kuhimiza uhusiano huo wenye msingi wa uratibu, ushirikiano na utulivu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako