• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: China yafanya uwekezaji mkubwa Tanzania

  (GMT+08:00) 2018-12-05 19:45:19

  Jumla ya miradi ya uwekezaji 905 imesajiliwa nchini katika kipindi cha miaka mitatu nchini Tanzania.

  Kati ya miradi hiyo, 307 ni ya Watanzania, 319 ya wawekezaji kutoka nje na 277 ni ya ubia kati ya Watanzania na wageni.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Godfrey Mwambe amesema miradi yote hiyo ina thamani ya dola za Marekani 13.2 bilioni.

  Alisema kati ya miradi hiyo, 478 ni ya viwanda, huku uwekezaji mkubwa ukifanywa na nchi ya China.

  Mwambe alisema miradi hiyo ni ile ambayo imefikia vigezo vya kusajiliwa na TIC ambayo kwa mwekezaji wa ndani mtaji wake ni dola za Marekani 100,000 wakati mwekezaji wa nje ni dola 500.000.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako