• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Watendaji wa Serikali watakiwa kuondoa mazingira ya urasimu

  (GMT+08:00) 2018-12-05 19:45:36

  Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amewataka watendaji wa Serikali kuondoa mazingira ya urasimu yanayosababisha kukwama kwa shughuli za uwekezaji.

  Majaliwa alitoa agizo hilo alipotembelea Kituo cha Taifa cha Uwekezaji (TIC) ikiwa ni mara ya kwanza tangu kihamishiwe chini ya ofisi yake kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.

  Pamoja na kuzungumza na wakurugenzi na watendaji wa kituo hicho, Majaliwa alitembelea kituo cha pamoja cha utoaji huduma kinachokusanya idara zote za Serikali.

  Ameagiza kufanyike marekebisho ili kuondoa ukinzani wa sheria zinazoratibu utendaji kazi wa idara na taasisi za Serikali zinazohusika na uwekezaji.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako