• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Huduma za kutalii Rwanda zazinduliwa kwenye mitandao ya huduma za utalii China

  (GMT+08:00) 2018-12-06 08:50:20

  Huduma za kutalii nchini Rwanda zimezinduliwa rasmi kwenye moja ya majukwaa ya mtandaoni ya huduma za utalii nchini China, hatua ambayo itawawezesha watalii wa China kuchagua moja kwa moja safari ya kutalii Rwanda.

  Taarifa iliyotolewa jana na Bodi ya maendeleo ya Rwanda RDB imesema kuzinduliwa kwa ukurasa wa Rwanda kwenye tovuti ya huduma za utalii ya Alibaba, Fliggy, kunafuatia uzinduzi wa Jukwaa la kielektroniki la biashara duniani (eWTP) la China mwezi Oktoba, ambalo linalenga kuhimiza mawasiliano kati ya sekta za umma na binafsi.

  Kwa mujibu wa makubaliano yaliyosainiwa kati serikali ya Rwanda na kampuni ya Alibaba chini ya mfumo wa eWTP, Fliggy na RDB watashirikiana katika kutangaza utalii wa Rwanda nchini China, kwa kupitia Duka la mtandaoni la utalii wa Rwanda, ambalo watalii wanaweza kuagiza safari za ndege, hoteli na kubadilishana uzoefu wa utalii, pamoja na Ukurasa wa Rwanda unaowawezesha watalii wa China kuifahamu zaidi nchi hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako