• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya inataka kutumia teknolojia ya viwanda ya China ili kuhimiza uuzaji bidhaa nje

  (GMT+08:00) 2018-12-06 09:10:04

  Jumuiya ya wafanyabiashara wa Kenya inataka kutumia teknolojia ya viwanda ya China ili kuhimiza uuzaji wa bidhaa zake nje ya nchi. Akiongea mjini Nairobi kwenye maonyesho na kongamano la biashara kati ya China na Kenya, makamu mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara na wenye viwanda cha Kenya (KNCCI) Bw. James Mureu, amesema wanapenda kuwa na ubia na makampuni ya China ili Kenya iweze kunufaika na teknolojia ya viwanda ya China na kuifanya Kenya iwe muuzaji mkubwa wa bidhaa nje.

  Mkurugenzi wa biashara ya pande mbili katika wizara ya biashara ya Kenya Bibi Oliver Konje, amesema maonyesho yanatoa jukwaa zuri kwa wateja wa Kenya kushirikiana na wauzaji wa China. Amesema Kenya inakaribisha ongezeko la uwekezaji wa China nchini Kenya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako