• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri wa mambo ya nje wa China afanya majumuisho ya ziara za rais Xi Jinping nchini Hispania, Argentina, Panama na Ureno

  (GMT+08:00) 2018-12-06 09:33:25

  Kuanzia tarehe 27 Novemba hadi Disemba 5, rais Xi Jinping wa China alifanya ziara za kitaifa nchini Hispania, Argentina, Panama na Ureno na pia kushiriki kwenye mkutano wa 13 wa kilele wa viongozi wa kundi la G20 uliofanyika mjini Buenos Aires. Baada ya ziara hizo kumalizika, waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi amefanya majumuisho ya ziara za rais Xi.

  Bw. Wang amesema ziara hizo zimehimiza ushirikiano wa nchi za kundi la G20 na kupanga maendeleo ya uhusiano kati ya nchi kubwa, zimeinua ngazi ya ushirikiano kati ya China na Hispania na Ureno na kuingiza uhai mpya kwenye uhusiano kati ya China na Ulaya, zimeimarisha uhusiano kati ya China na Argentina na Panama na kuboresha mpango wa ushirikiano kati ya China na nchi za Latin Amerika, na pia zimefafanua fikra za China, na kuonyesha sura ya China inayojiamini na yenye uvumilivu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako