• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • UM washtushwa na ukatili wa kingono dhidi ya wanawake Sudan Kusini

  (GMT+08:00) 2018-12-06 09:43:20

  Maofisa waandamizi wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika wameshutushwa na ripoti kuhusu matukio ya ukatili wa kingono dhidi ya wanawake na wasichana zaidi ya 150 yanayotokana na migogoro nchini Sudan Kusini, na kuitaka serikali ya nchi hiyo ichukue hatua za kukabiliana na vitendo hivyo.

  Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema katika zaidi ya siku 10 zilizopita, mashambulizi dhidi ya wanawake na wasichana yalitokea wakati walipokuwa wakisafiri kutoka kwenye vijiji vyao kwenda mjini Bentiu katika jimbo la Unity linalodhibitiwa na serikali. Amesema naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia operesheni za ulinzi wa amani Bw. Jean-Pierre Lacroix, kamishna wa Umoja wa Afrika anayeshughulikia mambo ya amani na usalama Bw. Smail Chergui, naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mambo ya wanawake Bibi Phumzile Mlambo-Ngcukaz wameshtushwa na matukio hayo ya ukatili wa kingono, ukiwemo ubakaji.

  Habari nyingine zinasema Tume ya pamoja ya Usimamizi na Tathmini ya Sudan Kusini JMEC imeanza kuchunguza matukio hayo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako