• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • FAO yatoa wito wa kutoa mbolea zisizo na uchafuzi kwenye udongo

  (GMT+08:00) 2018-12-06 17:03:32

  Mkurugenzi wa Ofisi ya Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) mjini New York Bi. Carla Mucavi ametoa wito wa kuvumbua njia za kuzalisha mbolea ambazo hazitakuwa na madhara kwa udongo au madini makali ya chuma.

  Akizungumza kwenye Siku ya Kimataifa ya Udongo, Bi. Mucavi amesema udongo bora ni muhimu sana katika kutimiza ajenda ya mwaka 2030 ya maendeleo endelevu, na kutimiza malengo ya kumaliza umasikini, kuondoa njaa na kuhakikisha maji safi na salama. Amesema mpaka kufikia mwaka 2015, asilimia 33 ya ardhi ilikuwa imepunguza rutuba kutokana na mmomonyoko wa udongo, kuongozeka kwa chumvi, na uchafuzi unaotokana na kemikali.

  Mkurugenzi huyo amesifu juhudi zinazofanywa na Kundi la China la Kingenta ambalo linatengeneza mbolea zinazoboresha uzalishaji huku zikilinda udongo, na kusema uzalishaji wa aina hii ya mbolea unapaswa kuongezwa zaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako