• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waatalamu waona kuwa China imeonesha umuhimu mkubwa katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa

  (GMT+08:00) 2018-12-06 17:09:28

  Mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa ya Umoja wa Mataifa unaendelea kufanyika mjini Katowice, Poland. Baadhi ya wataalamu wanaohudhuria mkutano huo wanaona mafanikio iliyopata China katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa yanafuatiliwa na watu, na kuchangia katika mchakato wa ushirikiano wa kimataifa. Pia wanaona nchi zinazobeba majukumu muhimu ya kihistoria na zile zilizotoa kwa wingi zaidi hewa zinazoleta ongezeko la joto duniani, zinatakiwa kubeba majukumu makubwa zaidi.

  Mkutano huo wa mabadiliko ya hali ya hewa ni muhimu zaidi tangu Makubaliano ya Paris yaliposainiwa, na pande mbalimbali zitaanzisha mazungumzo kuhusu kanuni halisi za makubaliano hayo, na kufikia maafikiano ili kutekeleza kwa ufanisi makubaliano hayo.

  Majukumu katika kupunguza utoaji wa hewa zinazosababisha ongezeko la joto duniani ni jambo muhimu liliko kwenye Makubaliano ya Paris. Mtandao wa Nchi zinazoendelea duniani (third world network) ni kituo kisicho cha kibiashara cha washauri bingwa kinachoshughulikia masuala kuhusu uchumi na mazingira ya dunia. Mshauri wa sheria na mratibu wa Mtandao wa Nchi zinazoendelea duniani Bibi Meenakshi Raman anaona kuwa, majukumu yanayobebwa na nchi zilizoendelea na zile zinazoendelea zinatakiwa kutofautishwa. Tangu mapinduzi ya viwanda yalipotokea, nchi zilizoendelea duniani zimetoa hewa za Carbon Dioxide bila ya ukomo, hali ambayo imesababisha matatizo ya hali ya hewa yanayomkabili binadamu. Bibi Raman anasema:

  "Sasa tunakabiliwa kwa pamoja changamoto ya hali ya hewa, lakini nchi zilizoendelea na zile zinazoendelea zinatakiwa kubeba majukumu tofauti. Zile zilizotoa kwa wingi hewa zinazosababisha ongezeko la joto duniani zinatakiwa kubeba majukumu makubwa zaidi na kufanya kazi ya uongozi."

  Naibu mkurugenzi wa Kamati ya wataalamu wa hali ya hewa ya China Prof. He Jiankun ameeleza kuwa, Makubaliano ya Paris yamesisitiza kanuni za kubeba majukumu ya pamoja lakini kwa namna tofauti, kuwepo kwa usawa na kubeba majukumu kwa mujibu wa uwezo wa nchi, na pia kuzingatia hali tofauti ya nchi mbalimbali, ambazo ziliwekwa kwenye Makubaliano ya mfumo wa hali ya hewa ya Umoja wa Mataifa. Katika miaka ya hivi karibuni, mafanikio iliyopata China katika kupunguza utoaji wa hewa zinazosababisha ongezeko la joto duniani, na kutekeleza ahadi zao katika nyanja hiyo yamefuatiliwa na watu duniani, na China imetimiza ahadi yake ya kupunguza utoaji wa hewa hizo kwa asilimia 40 hadi 50, miaka mitatu kabla ya mwaka 2020 kama ilivyopangwa. Bw. He Jiankun anasema:

  "Kadiri uchumi wa China unavyokua kwa kasi, ndivyo utoaji wa jumla wa hewa za Carbon Dioxide unavyoongezeka, lakini kiwango cha utoaji huo kwa GDP kimepungua. Kiwango hicho kinalingana na hali ya China ikiwa nchi inayoendelea, ambacho kinakubalika kwa jumuiya ya kimataifa duniani."

  Bw. He Jiankun pia amesisitiza kuwa, China imeonesha umuhimu mkubwa katika ushirikiano wa ndani na wa kimataifa katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako