• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Russia yasema uhusiano wa kirafiki kati yake na China hauamuliwi na mambo ya nje

  (GMT+08:00) 2018-12-06 17:10:53

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Russia Bi. Maria Zakharova jana amesema, Russia na China zinatilia maanani sana uhusiano wa kirafiki kati yao, na uhusiano huo hauamuliwi na mambo ya nje.

  Akizungumzia mkutano wa viogozi wa nchi hizo mbili wakati wa mkutano wa kilele wa kundi la nchi 20 (G20), Bi. Zakharova amesema, uhusiano wa kirafiki kati ya Russia na China hauamuliwi na hali ya kimataifa na hali ya kikanda. Amesema mipaka, jiografia, historia na maslahi ya wananchi zinaufanya uhusiano kati ya nchi hizo jirani uwe wa karibu zaidi.

  Bi. Zakharova amesema China ni mshiriki wa kuwajibika wa mambo ya kimataifa, na katika mazingira ya kimataifa ya hivi sasa yasiyo na utulivu, mazungumzo kati ya washiriki wa kuwajibika wa mambo ya kimataifa ni muhimu sana.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako