• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yasema jumuiya ya kimataifa inatakiwa kuimarisha uhusiano wa kiwenzi wa maendeleo ya dunia ili kuhimiza amani endelevu

  (GMT+08:00) 2018-12-06 18:07:52

  Balozi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Ma Zhaoxu amesema, umaskini na ukosefu wa maendeleo ni chanzo kikuu cha mapigano, hivyo jumuiya ya kimataifa inatakiwa kutekeleza kwa pande zote ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030, kuimarisha uhusiano wa kiwenzi wa maendeleo ya dunia na kutimiza ahadi za utoaji wa msaada, ili kuhimiza amani ya kudumu kupitia maendeleo endelevu.

  Bw. Ma amesema hayo katika Mjadala wa Umoja wa Mataifa wenye kauli mbiu ya "Kujenga na kudumisha amani: ujenzi mpya, amani, usalama na utulivu baada ya mapigano." Amesema, baada ya mapigano, nchi zinakabiliwa na majukumu muhimu ya kuendeleza uchumi, na kusema amani itaimarishwa na mapigano yataepushwa kama wananchi wakipata ajira na kuishi maisha mazuri.

  Akizungumzia ujenzi mpya baada ya mapigano, Balozi Ma amesema kuwa jumuiya ya kimataifa inatakiwa kufuata mkataba wa Umoja wa Mataifa na kanuni za msingi za uhusiano wa kimataifa, kuheshimu mamlaka ya nchi iliyokumbwa na mapigano na kuisaidia kutafuta njia ya maendeleo inayoendana na hali ya nchi hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako