• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yazitaka pande mbalimbali za Yemen kuchukua nafasi zao kufanya mazungumzo yenye ufanisi na udhati

  (GMT+08:00) 2018-12-06 18:08:09

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang hapa Beijing amesema, China inazitaka pande mbalimbali za Yemen kutilia maanani maslahi ya taifa na wananchi, na kuchukua nafasi zao na kufanya mazungumzo kwa msimamo wa ufanisi na udhati, ili kujenga mazingira na masharti mazuri kwa kurejesha amani, utulivu na utaratibu nchini humo mapema iwezekanavyo.

  Habari zinasema, ujumbe wa serikali ya Yemen na ujumbe wa kundi la Houthi jana umewasili nchini Sweden, na mazungumzo ya amani yanatarajiwa kufanyika haraka. Hii itakuwa mara ya kwanza kwa pande mbili zinazopingana za Yemen kufanya mazungumzo ya amani uso kwa uso.

  Bw. Geng amesema, China inapongeza mazungumzo hayo na juhudi zilizofanywa na mjumbe maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia suala la Yemen Bw. Martin Griffiths na pande husika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako