• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ziara ya rais wa China yafungua dirisha la kunufaishana lenye matumaini kwa dunia yenye ncha nyingi

  (GMT+08:00) 2018-12-06 19:03:50

  Rais Xi Jinping wa China amerejea Beijing baada ya kumaliza ziara katika nchi nne za Ulaya na Latin Amerika na kuhudhuria mkutano wa kilele wa G20. Akizungumzia ziara hiyo, Rais Xi amesema, ameona matarajio makubwa na matumaini mema ya watu wa nchi mbalimbali kuhusu amani na utulivu wa dunia, maendeleo na ustawi wa taifa na maisha mazuri. Rais Xi amesema, ingawa dunia inakabiliwa changamoto mbalimbali, China itaendelea kushikilia kanuni ya kuheshimiana, mazungumzo yenye usawa, maendeleo ya amani na ushirikiano wa kunufaishana, ili kufanya juhudi pamoja na nchi mbalimbali kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja.

  Changamoto zinazoikabili dunia zinatakiwa kutatuliwa kupitia mazungumzo kati ya nchi mbalimbali. Kwa kupitia ziara hiyo ya mwisho ya mwaka huu ya rais Xi, China imeendelea kusikiliza kwa dhati sauti za nchi mbalimbali, kutatua matatizo kupitia mazungumzo na nchi mbalimbali, kutoa mapendekezo yanayounga mkono mfumo wa pande nyingi na kuhimiza ushirikiano wa kunufaishana, huku ikiendelea kuonesha majukumu ya nchi kubwa.

  Katika taarifa zilizotolewa kwa nyakati tofauti na China na Hispania, Argentina, Panama na Ureno, pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" la China limeungana na mikakati ya nchi hizo nne, na chini ya utaratibu huo pande hizo zimeanzisha mawasiliano na ushirikiano katika soko la upande wa tatu, na kutimiza ushirikiano wa kunufaishana katika eneo kubwa zaidi.

  Katika mikutano mingi kati ya pande mbili au pande nyingi, rais Xi akiwa kiongozi wa nchi kubwa zaidi inayoendelea duniani, ameeleza msimamo wa nchi zinazoendelea ambao unajumuisha maoni ya pande nyingi, huku akipendekeza kuwa biashara ya kimataifa inatakiwa kushikilia mwelekeo wa miaeneo matatu ya "Uwazi, Uvumilivu na Kanuni". Ameongeza kuwa usimamizi wa uchumi wa dunia unatakiwa kuweka kipaumbele katika suala la maendeleo, kushikilia ushirikiano wenye uwazi, moyo wa kiwenzi, uongozaji wa uvumbuzi na ushirikiano wa kunufaisha wa pande zote.

  Wakati dunia ikiaga mwaka 2018, ziara hiyo ya rais Xi imehimiza ujenzi wa pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja", kuzidisha uhusiano na moyo wa kiwenzi na kushiriki kwenye mchakato wa usimamizi wa dunia. Kwa kukabiliana na matumaina na matarajio ya watu wa nchi mbalimbali, dunia pia inahitaji viongozi wengi zaidi kuonesha uimara, uelewa, na wanaobeba majukumu katika hali yenye mabadiliko mbalimbali.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako