• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya Airways yapunguza safari za moja kwa moja kati ya Nairobi na Newyork

  (GMT+08:00) 2018-12-06 20:44:44

  Shirika la ndege la Kenya Kenya Aiways limetangaza kupunguza safari zake za moja kwa moja mjini New York kutoka saba hadi tano kwa wiki. Shirika hilo limesema safari hizo zitakuwa siku za Jumanne, Alhamisi, Ijumaa ,Jumamosi na Jumapili.Katibu mkuu mtendaji wa shirika hilo Bw Sebastian Mikosz amesema uamuzi huo ni wa kibiashara na kusisitiza kuwa bado shirika hilo limejitolea kuhakikisha kuwa wateja wake wanafurahia safari za miji hiyo hiyo miwili. Sebastian ameongeza kuwa watapitia upya uamuzi huo kuona kama wataanza tena safari za moja kwa moja kila siku kati ya miji ya Nairobi na New York.Taarifa ya hapo awali ilikuwa ikisema kuwa hatua hiyo inatokana na kupungua kwa wateja wa shirika hilo wanaosafiri kati ya miji hiyo miwili.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako