• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Brookside kuanza kulipa wakulima kulingana na ubora wa maziwa yao

  (GMT+08:00) 2018-12-06 20:45:32

  Kampuni ya maziwa ya Brookside nchini Kenya imesema itaanza kuwalipa wakulima kulingana na ubora wa maziwa yao.

  Mkurungezi wa kampuni hiyo Muhoho Kenyatta amesema hatua hiyo itasaidia kuzalisha bidhaa nyingine za hali ya juu zitokanazo na maziwa kama vile siagi.

  Mpango huo wa kutoa bei kulingana na ubora utategemea kiasi cha siagi katika kilo ya maziwa ghafi na maziwa yasio na kemikali au maji.

  Hatua hiyo mpya ni tofauti na awali ambapo wakulima walilipwa kulingana na uzani wa maziwa yao bila kuzingatia ubora.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako