• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Wafanyabiashara Tanzania kutangaza msimano wao kuhusu kodi

  (GMT+08:00) 2018-12-06 20:45:51

  Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini Tanzania imeahirisha kikao kati yake na wafanyabiashara kilichokuwa na lengo la kuunga mkono kauli ya Rais John Magufuli kuhusu ukusanyaji kodi.

  Mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Siliver Kiondo amesema kwenye viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam kuwa, kikao hicho kingekuwa cha wazi lakini kimeahirishwa kwa sababu za usalama.

  Amesema kikao hicho kitafanyika kesho na watatoa tamko la kuunga mkono kauli ya Rais Magufuli sanjari na kutoa madukudku yao.

  Kiondo amesema kuwa lengo leo sio kuleta vurugu bali kusoma tamko kwa nia ya kuboresha utendaji kazi wao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako