• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rwanda: IFC na I&M zasaini mkataba wa miaka miwili

  (GMT+08:00) 2018-12-06 20:46:08

  Shirika la fedha la Kimataifa IFC limesaini mkataba wa miaka miwili wa kutoka ushauri kwa benki ya I&M nchini Rwanda kuhusu utoaji wa mikopo kwa biashara ndogo ndogo na zile za wastani.

  Mkataba huo unafuatia mkopo wa dola milioni 10 uliotolewa na IFC kwa benki hiyo mwezi Mei mwaka huu.

  Mkurungezi wa benki hiyo Robin Bairstow, amesema mkopo na ushirikiano huo zitasaidia kufikisha huduma kwa wateja zaidi.

  Biashara ndogo na za wastani zinachukua asilimia 98 ya biashara zote nchini Rwanda na huchangia zaidi ya nusu ya pato la kitaifa.

  Lakini hata hivyo biashara hizo zinakabiliwa na matatizo ya mitaji huku kukiwa na mwanya wa upatikanaji wa mikopo wa dola bilioni 1.2.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako