• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Shilingi bilioni 40 zatumika kununua korosho Tanzania

  (GMT+08:00) 2018-12-06 20:47:05

  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji wa Tanzania Joseph Kakunda amesema zaidi Sh40 bilioni zimetumika kununua korosho kwa wakulima 40,000 kati ya Sh528 bilioni zinazotarajiwa kununua tani 160,000 zilizopo katika maghala.

  Kakunda ameyasema hayo jijini Dar es Salaam alipotembelea maonyesho ya bidhaa za viwandani ambayo yamefunguliwa rasmi leo katika viwanja vya Sabasaba.

  Amesema tani 275,000 za korosho zinatarajiwa kuvunwa msimu huu na mpaka sasa tayari wakulima wamevuna na kuuza tani 160,000 na tani nyingine 100,000 zikitarajiwa kuvunwa mwezi huu.

  Serikali nchini humo hivi karibuni imeendelea kuchukua hatua za kuwalinda wakulima wa korosho kwa kuwahakikishia bei bora na kuondoa madalali.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako