• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mawasiliano na ushirikiano kati ya ujumbe wa uchumi na biashara wa China na Marekani yaendelea vizuri

  (GMT+08:00) 2018-12-06 20:53:30

  Msemaji wa Wizara ya biashara ya China Bw. Gao Feng amesema, hivi sasa mawasiliano na ushirikiano kati ya ujumbe wa uchumi na biashara wa China na Marekani yanaendelea vizuri, na China ina imani juu ya kufikiwa kwa makubaliano ndani ya siku 90 zijazo.

  Bw. Gao Feng amesema, mazungumzo kati ya viongozi wa China na Marekani nchini Argentina yamefikia maafikiano muhimu kuhusu masuala ya uchumi na biashara. Katika kipindi kijacho pande hizo mbili zitatekeleza makubaliano yaliyofikiwa katika sekta za mazao ya kilimo, nishati na magari.

  Pia amesisitiza kuwa pande hizo mbili zitachukua hatua ya kufuta ushuru wote ulioongezwa ndani ya siku 90 zijazo kuwa lengo la mwisho, pia zinafanya juhudi za kufikia makubaliano kuhusu masuala muhimu kwa kufuata msingi wa kuheshimiana, kunufaishana na kuzingatia ufuatiliaji wa pamoja.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako