• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika Kusini yazindua eneo maalumu la kiuchumi karibu na Cape Town

    (GMT+08:00) 2018-12-07 08:49:46

    Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika kusini amezindua Eneo maalum la kiuchumi la Atlantis nje ya mji wa Cape Town, na kufanya idadi ya maeneo maalumu ya kiuchumi nchini humo ifikie tisa.

    Akiongea kwenye sherehe ya uzinduzi, rais Ramaphosa amesema eneo hilo linachukuliwa kuwa ni hatua ya kuhimiza maendeleo endelevu ya kiuchumi kwenye kanda yenye mustakbali mzuri inayokabiliwa na changamoto za kijamii.

    Msingi mkuu wa eneo maalumu la Atlantis ni kufichua thamani ya kiuchumi isiyoonekana ya miundombinu iliyopo na isiyotumika kikamilifu, kupitia kujenga kituo hicho cha kuzalisha bidhaa kwa teknolojia safi.

    Amesema katika kipindi kifupi kijacho, eneo hilo la Atlantis linatarajiwa kutoa nafasi za ajira zaidi ya 1,400.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako